Sunday, August 28, 2011

Uhaba wa wafanya kazi Iringa.

UHABA wa Wafanyakazi na ukosefu wa vitendea kazi katika Idara ya Misitu Manispaa ya iringa, yasababisha uharibifu wa mazingira kwa wananchi wa manispaa kukata miti ovyo.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa Theresia Mahongo, alipokuwa akizungumza na kituo hiki Ofisini kwake Mwishoni mwa wiki iliyopita .

Amesema kuwa idara hiyo inawafanyakazi 3 wanaotakiwa kuzunguka katika maeneo yote kutoa elimu na kuhakikisha matumizi mabaya ya mazingira hayatokei.


Mahongo amesema kuwa kumekuwa na uharibifu mkubwa katika maeneo yote yanaozunguka mto Ruaha, kwa wananchi kukata miti kwa ajili ya kuchomka mkaa na pia kuchoma tofali.


Hata hivyo amesema kuwa idara hiyo inakabiliwa na ukosefu wa vitendea kazi, hivyo humpa wakati mgumu mtumishi huyo kuweza kufanyakazi kwa wakati, na matokeo yake kutoa mwanya kwa waharibifu wakidhani kuwa hakuna sheria ya kuwabana.
 

Kwa upande wake Meya wa Manispaa hiyo Aman Mwamwindi, amesema kuwa umefika wakati wa kushirikiana katika kutunza mazingira na kila mtu kujituma kuhakikisha uharibifu wa mazingira hauendelea hata pale ambapo hayupo mtumishi wa serikali.

ABUJA

Watu 20 wamefariki dunia nchini Nigeria baada ya mvua kubwa iliyonyesha nchini humo tangu Ijumaa, kusababisha bwawa moja kufurika na kuzamisha nyumba kadhaa, kusini magharibi mwa nchi hiyo.


Msemaji wa shirika linaloshughulikia majanga ya dharura nchini humo, Yushau Shuaib amethibitisha vifo hivyo, vilivyosababishwa na mafuriko katika mji wa Ibadan.


Vyombo vya habari nchini humo vimearifu kuwa maelfu ya watu wamekimbia makaazi yao, na kwa mujibu wa Shuaib, kwa sasa ni vigumu kupata idadi kamili ya watu waliyoyahama makaazi yao.

Friday, August 26, 2011

Waasi wa Libya ni Hatari.

Waasi wa Libya wadhibiti kituo cha ukaguzi mpakani na Tunisia
muammar gaddafi
Wapiganaji waasi katika operesheni
Vikosi vya waasi wa Libya, vinaripotiwa kudhibiti kituo cha ukaguzi cha Ras Jdir kwenye mpaka wa Libya na Tunisia.
Vyanzo mbalimbali vya habari vimewanukuu mashahidi waliosema kuwa waasi wameudhibiti mpaka huo baada ya kupambana na wanajeshi wanaomuunga mkono kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi.


Mpaka huo upo kwenye barabara muhimu ya pwani inayotokea Tunisia hadi Tripoli nchini Libya. Mwandishi habari wa DW Martin Fletcher alie Tripoli hivi sasa, anasema waasi wanafanya kila liwezekanalo kumkamata Gaddafi. Inadhaniwa kwamba Gaddafi amekimbilia mji alikozaliwa wa Sirte.
gaddafi bodyguards


Mji huo ulilengwa na ndege za kivita za NATO asubuhi ya hapo jana. Wakati huohuo Umoja wa Afrika umesema hautolitambua Baraza la Mpito la waasi kama chombo halali kinachowakilisha Libya, ilimradi mapigano yanaendelea nchini humo.

Thursday, August 25, 2011

Watatu wakamatwa na Kete za Bangi.

Watu watatu wakamatwa na kete 108 za bangi mtaa wa tukuyu wilayani Mbozi, walikamatwa na askari mwenye namba E3843 Kikosi cha upelelezi anayeitwa Greyson na wenzake wakiwa doria.
Waliokamatwa ni Joshua Mwanange(25) mkazi wa Tukuyu, Frank Simfukwe (19) Mkazi wa Tukuyu Tunduma na Juma Charles (20) mkazi wa Tukuyu Tunduma wote kwa pamoja wamekamatwa na kete hizo zenye uzito wa kilo gramu 500.


Watuhumiwa wapo mahabusu wilayani Mbozi watafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezoi kumilika.

Kikongwe alala na Maiti


KIKONGWE mwenye umri wa miaka 85 aliyefahamika kwa jina la Sadiki Salehe mkazi wa Ilolo kata ya Ruanda Jijini Mbeya amejikuta matatani kufuatia kulala na maiti ya mtoto wake pekee kwa siku sita.



Habari za kuaminika kutoka kijijini hapo zimesema kuwa wakati harufu hiyo ikiendelea kuzagaa eneo la nyumba yake na majirani, Kikongwe huyo alikuwa akiendelea kuandaa futari karibu na mlango wa chumba cha marehemu hasa ukizingatia huu ni mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Mtoto wa kikongwe huyo alijulikana kwa jina la Salehe Sadiki(38) kwa mara ya mwisho alionekana Jumatano ya wiki liliopita(Agosti 17, 2011).

Kikongwe huyo alipohojiwa alisema kuwa Jumatano ya Agosti 24 mwaka huu akiwa nyumbani kwake alikuwa anahitaji dishi la kuogea ambalo lilikuwa katika chumba cha marehemu ambaye alikuwa akiishi nje ya nyumba ambayo ilikuwa ikitizama na ya baba yake umbali wa meta 1.5.
Na mara baada ya kuchukua hatua ya kutaka dishi hilo ndipo alipoenda na kugonga mlango wa chumba cha marehemu na kukuta mlango ukiwa umefungwa huku harufu ikitoka kwa mbali.

Harufu hiyo ilimshtua kikongwe huyo ambaye aliamua kwenda msikiti wa Soweto uliopo Jijini Mbeya kwa Imamu Eliasa Selemani ambaye naye alimtaarifu balozi wa mtaa huo Iddi Malole kuhusu tukio hilo.

Imamu Eliasa na Balozi Malole kwa pamoja walimtaarifu Mwenyekiti wa Mtaa wa Ilolo Benson Mbwana kuhusu tukio hilo la kushangaza ambaye alimua kutoa taarifa katika kituo cha Polisi Mwanjelwa.

Kituo cha Polisi cha Mwanjelwa kilishindwa kushughulikia suala hilo ambalo lilipelekwa katika kituo cha Polisi cha Kati (CENTRAL POLICE) ambacho kiliruhusu kuzikwa kwa mwili huo ambao ulikuwa umeharibika vibaya kwa kupasuka huku Polisi ikiendelea na uchunguzi wa tukio hilo.

Wakati Polisi wakitoa amri ya kuzikwa kwa mwili huo wakazi wa mtaa huo walipandwa na hasira kufuatia tukio hilo na walisikika wakisema kuwa sio mara ya kwanza kwa mzee huyo ambaye hapo awali alimuua mkewe na kumweka uvunguni mwa kitanda kwa zaidi ya siku nne hali iliyomfanya atumikie kifungo cha zaidi ya miaka 8 jela kutokana sakata hilo.

Polisi walipoona hayo ilimuondoa mzee huyo eneo la tukio kwa nguvu ili kunusuru maisha yake.

Wakati polisi ikiondoka na mzee huyo wakazi hao walisikika wakisema mzee huyu hatakiwi kurudi tena kijijini hapo kutokana na vitendo hivyo

ATAKAYE KATISHA KATIKA UWANJA licha ya sura yake ya upole aliyonayo na kushinda msikitini.

Aidha Mwenyekiti wa mtaa huo alisema sula hilo sasa limo mikononi mwa Jeshi la Polisi hivyo watalishughulikia ipasavyo.

Friday, August 19, 2011

Iringa,Mafinga na Songea.


Happy Birthday Brother

Agape Msumari.

anusurika kifo sababu ya Uchawi.

Nidhana potofu walizojijengea baadhi ya watanzania hususani waishio Vijijini baada yakuona mtu mwenye umri mkubwa (yaani mzee) na kuona kuwa anamacho mekundu nakukosa shughuli ya kufanya huisiwa kuwa ni wachawi, tatizo hili nikubwa kwa jamii yatu ya Tanzania kama nilivyosema hapo hawali.
Moja kati ya watu waliokumbwa na tatizo hili ni mama huyu. (anayeonekana kwenye picha)

Mwana mke huyu ni mkazi wa kijijini na mtu aliyetaka kumdhuru ni mtoto wake wakwanza kumzaa ambaye ni mwanaume anayejishughulisha na kilimo kijijini hapo kijana huyo niliyemtambua kwa jina la Mohamed.
Chakusikitisha zaidi ni kwamba mwenyekiti wakijiji hakuwa na taarifa hizo na kustushwa na tukio hilo ambalo lilitokea asubuhi na mtoto wake wakike ndiye aliyenusuru maisha ya mama huyo baada yakupiga kelele na kuwaita majirani kumnusumu mama yao.
Kisa cha mtoto huyo kutaka kumuua mama yao ni baada ya kufariki mtoto wake wakike nakuhisi kuwa mama yake ameshiriki tukio la kifo cha mtoto wake.
na hii ni video yake akiwa anajieleza mama huyo




Thursday, August 18, 2011

Vituko vya Dar.

Choo cha kupanda hicho jamni nimekikuta maeneo ya mchikichini kama unapafahamu ni karibu na jangwani nilipokuwa kwenye matembezi nikakutana na hali hiii duh! kweli duniani kuna mambo hapo kuna watu wapo mahali na kujisifia kuwa wapo Dar na hiki ndicho choo anachotumia.
Hii ni poolltable kama unavyojionea na kulipia ni kama kawaida kitambaa kimechanika kabisaaaa ni maeneo ya kigogo baada ya kutembelea nikaona watu wanacheza nami ilibidi nilipie na nisubiri watu waliokuwa wakicheza wamalize ili nami nicheze kwa gharama ya shs 200/= ya kitanzania japo halina ubora hata kidogo. hivi kweli nivituko.
Huyu kijana kama unavyomuona kwenye hii picha hapoa akiwa anamalizia kuruka ukuta baada ya kuchelewa kufika shule akaamua kuzunguka nyuma ya shule na kuruka ukuta ndipo alipokumbana na camera ya bongo120 akiwa anamalizia kuruka ukuta wa shule ambayo jina nimeliifadhi.

Mgambo wakamatwa na Rushwa.

Kuna wadada wawili jana mida ya saa saba mchana wamekamatwa kwa kosa la kupokea Rushwa kwa moja kati ya wafanyabiashara maeneo ya stend ya Ubungo ndani. kwa kawaida wadada hao ambao nilifanikiwa kujua kwa kajina yao ya Anna n Asia walikamatwa kwa kosa lakupokea Rushwa na kusemekeana kuwa ni kawaida ya wadada hao kupokea Rushwa maeneo hayo kwa kutumia uongozi walionao wa askari Jiji.
Kupitia picha hizi utajionea nakutambua nn kilitokea maeneo hayo ya Ubungo hapo anaonekana afsa wa TAKUKURU akijaribu kuwatuliza wananchi ili wasibanye fujo aada ya kuwakamata wadada hao 
(ambao hawaonekani wamekaa kwa chini)
kama unavyojionea hapo wadada hao Asia na Anna wakiongozwa na askari kuelekea kituo cha polisi.
Ni sehemu ya watu wakiandamani kuwasindikiza watuhumiwa na wengine ni wasafiri wa mikoani wakiwa wamekatisha shughuli zao hili kushuhudia tulio hilo.
msafala uliishia hapo jamani.

Mr Aliisi na maisha ya Music.

Moja kati ya watu ambao wamejikita kwenye Music toka Utotoni mpaka sasa na nimoja kati ya watu waliopata mafanikio makubwa katika Music jina analotumia ni Mr Aliisi na nimoja kati ya watu wanaotoa Elimu ya music katika chuo cha Music za SANAVUKA.
Mr Aliisi ni mzaliwa wa Nchini Kenya ila ni Mtanzania kwa sasa na pamoja na shughuli zake za music anazifanyia hapa Tanzania. check nae kwenye facebook (http://www.facebook.com/fredaliisi)