Thursday, August 18, 2011

Vituko vya Dar.

Choo cha kupanda hicho jamni nimekikuta maeneo ya mchikichini kama unapafahamu ni karibu na jangwani nilipokuwa kwenye matembezi nikakutana na hali hiii duh! kweli duniani kuna mambo hapo kuna watu wapo mahali na kujisifia kuwa wapo Dar na hiki ndicho choo anachotumia.
Hii ni poolltable kama unavyojionea na kulipia ni kama kawaida kitambaa kimechanika kabisaaaa ni maeneo ya kigogo baada ya kutembelea nikaona watu wanacheza nami ilibidi nilipie na nisubiri watu waliokuwa wakicheza wamalize ili nami nicheze kwa gharama ya shs 200/= ya kitanzania japo halina ubora hata kidogo. hivi kweli nivituko.
Huyu kijana kama unavyomuona kwenye hii picha hapoa akiwa anamalizia kuruka ukuta baada ya kuchelewa kufika shule akaamua kuzunguka nyuma ya shule na kuruka ukuta ndipo alipokumbana na camera ya bongo120 akiwa anamalizia kuruka ukuta wa shule ambayo jina nimeliifadhi.

No comments:

Post a Comment