Sunday, August 28, 2011

Uhaba wa wafanya kazi Iringa.

UHABA wa Wafanyakazi na ukosefu wa vitendea kazi katika Idara ya Misitu Manispaa ya iringa, yasababisha uharibifu wa mazingira kwa wananchi wa manispaa kukata miti ovyo.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa Theresia Mahongo, alipokuwa akizungumza na kituo hiki Ofisini kwake Mwishoni mwa wiki iliyopita .

Amesema kuwa idara hiyo inawafanyakazi 3 wanaotakiwa kuzunguka katika maeneo yote kutoa elimu na kuhakikisha matumizi mabaya ya mazingira hayatokei.


Mahongo amesema kuwa kumekuwa na uharibifu mkubwa katika maeneo yote yanaozunguka mto Ruaha, kwa wananchi kukata miti kwa ajili ya kuchomka mkaa na pia kuchoma tofali.


Hata hivyo amesema kuwa idara hiyo inakabiliwa na ukosefu wa vitendea kazi, hivyo humpa wakati mgumu mtumishi huyo kuweza kufanyakazi kwa wakati, na matokeo yake kutoa mwanya kwa waharibifu wakidhani kuwa hakuna sheria ya kuwabana.
 

Kwa upande wake Meya wa Manispaa hiyo Aman Mwamwindi, amesema kuwa umefika wakati wa kushirikiana katika kutunza mazingira na kila mtu kujituma kuhakikisha uharibifu wa mazingira hauendelea hata pale ambapo hayupo mtumishi wa serikali.

2 comments:

  1. haya bwana sasa tufanyaje kuovercome this problem

    ReplyDelete
  2. aiseee huku juu yaani umejipanga mwana...

    ReplyDelete