Sunday, August 28, 2011

ABUJA

Watu 20 wamefariki dunia nchini Nigeria baada ya mvua kubwa iliyonyesha nchini humo tangu Ijumaa, kusababisha bwawa moja kufurika na kuzamisha nyumba kadhaa, kusini magharibi mwa nchi hiyo.


Msemaji wa shirika linaloshughulikia majanga ya dharura nchini humo, Yushau Shuaib amethibitisha vifo hivyo, vilivyosababishwa na mafuriko katika mji wa Ibadan.


Vyombo vya habari nchini humo vimearifu kuwa maelfu ya watu wamekimbia makaazi yao, na kwa mujibu wa Shuaib, kwa sasa ni vigumu kupata idadi kamili ya watu waliyoyahama makaazi yao.

No comments:

Post a Comment