Friday, August 19, 2011

anusurika kifo sababu ya Uchawi.

Nidhana potofu walizojijengea baadhi ya watanzania hususani waishio Vijijini baada yakuona mtu mwenye umri mkubwa (yaani mzee) na kuona kuwa anamacho mekundu nakukosa shughuli ya kufanya huisiwa kuwa ni wachawi, tatizo hili nikubwa kwa jamii yatu ya Tanzania kama nilivyosema hapo hawali.
Moja kati ya watu waliokumbwa na tatizo hili ni mama huyu. (anayeonekana kwenye picha)

Mwana mke huyu ni mkazi wa kijijini na mtu aliyetaka kumdhuru ni mtoto wake wakwanza kumzaa ambaye ni mwanaume anayejishughulisha na kilimo kijijini hapo kijana huyo niliyemtambua kwa jina la Mohamed.
Chakusikitisha zaidi ni kwamba mwenyekiti wakijiji hakuwa na taarifa hizo na kustushwa na tukio hilo ambalo lilitokea asubuhi na mtoto wake wakike ndiye aliyenusuru maisha ya mama huyo baada yakupiga kelele na kuwaita majirani kumnusumu mama yao.
Kisa cha mtoto huyo kutaka kumuua mama yao ni baada ya kufariki mtoto wake wakike nakuhisi kuwa mama yake ameshiriki tukio la kifo cha mtoto wake.
na hii ni video yake akiwa anajieleza mama huyo




No comments:

Post a Comment