Wednesday, January 26, 2011
Tuesday, January 25, 2011
Toka juzi nilikuwa nafanya kazi hiii
hapa Ndio Shughuli ilikuwa ikianza kuelekea milimani kushoot video ya Filam itakayokuja kwa jina la "Siku moja utajua"
Hapa Mtoto wakiume nilikuwa nimeshaanza kazi niliyokuwa nimeitiwa
Huyu ndio Director wa move hiyo
Huyu anaitwa hamisi ndiye alikuwa kama zombi kwenye filam hiyo.
Huyunjamaa katika filam hiyo ameact kuwa amepikwa na kuuliwa na zombi hilo
Shughuli haikuishia hapo iliendelea mpaka usiku.
kupumzika nayo ilikuwepo
Chuo cha RUCO wafanya mgomo leo
Chuo cha Ruaha kilichopo Mkoani Iringa leo asubuhi wafanya mgomo na kuandamana kwa sababu ya kutaka Fedha zao za mikopo ambazo zinahusika na Bod ya mikopo.
hapa nikiwa nje ya Ofisi ya mkuu wa chuo kuingia nakuzungumza nae
Huyu ndio Mkuu wa chuo cha Ruaha Rev.Cephas Mgimwa hapa akizungumza ukweli na kujaribu kuweka uwazi kuwa fedha hizo zimesha toka na wanachosubiri ni majina ya wahusika wa Fedha hizo.
Hapa kama unavyojionea wanachuo wa Ruaha wakifanya maandamano hayo kuelekea ofisi ya Mkuu wa Chuo iliyopo chuoni hapo
Huku baadhi ya wanachuo hao wakifuatilia mgomo huo
Hapa nilijaribu kuzungumza na Raisi wa wanafunzi akijaribu kuelezea utaratibu wa fedha hizo,Huku wanachuo hao wakiwa hawako tayari kukubaliana na mazungumzo hayo zaidi ya kusisitiza upatikanaji wa fedha hizo za mikopo
Huyu ndio Mkuu wa chuo cha Ruaha Rev.Cephas Mgimwa hapa akizungumza ukweli na kujaribu kuweka uwazi kuwa fedha hizo zimesha toka na wanachosubiri ni majina ya wahusika wa Fedha hizo.
Monday, January 24, 2011
CAMERA YA BONGO120 WEEK HII.
HUYU NI ABBA NGILANGWA AKIWA KATIKA MAONGEZI.
SHANI AKIWA KATIKA MAANDALIZI YA KUANZA KIPINDI CHA SUNRISE POWER ASUBUHI
SHANI AKIWA KATIKA MAANDALIZI YA KUANZA KIPINDI CHA SUNRISE POWER ASUBUHI
HILI NI JEMBE LANGU SAG HAPA YUPO KWENYE KIPINDI CHA SUNRISE POWER AKISUBIRI KUFANYA MAJADILIANO NA KAMANDA WA POLICE.
Saturday, January 22, 2011
Friday, January 21, 2011
Tuesday, January 18, 2011
Sifa 10 muhimu Mwanaume anahitaji mwanamke awe nazo!
NINA imani afya yako msomaji wangu ni njema na tayari umeshafungua ubongo wako tayari kwa kupata chochote kutoka katika safu hii muruwa kwa ajili ya kuwekana sawa katika uhusiano wetu.
Naam! Najua utakuwa umesherehekea vyema Sikukuu ya Pasaka na pilikapilika za kujitafutia riziki za kila siku. Karibuni marafiki zangu.
Somo ambalo bado linaendelea kushika hatamu katika ukurasa huu, ni kama linavyoonekana hapo juu. Sifa ambazo wanaume wengi wanapenda wanawake wawe nazo.
Rafiki zangu, kila mwanaume anayetaka kuoa, huwa na sifa ambazo anatamani sana mwanamke wake awe nazo, kila mmoja ana sifa tofauti ambazo itategemea na utashi wake, lakini tafiti mbalimbali zilizowahi kufanywa na Wanasaikolojia wa Mapenzi, wamebaini sifa 10 ambazo wanaume wengi wanapenda wanawake wawe nazo.
Katika majuma mawili yaliyopita, nilianza kwa kuanisha sifa 5, kwa faida ya wale ambao hawakubahatika kusoma ni pamoja na mwenye mapenzi ya dhati, anayeheshimu thamani yake, mwenye heshima, anayejitambua na aliye mfariji, sasa tuendelee na sifa nyingine.
5. Mkarimu
Wanaume wanapenda sana kuishi na wanawake wakarimu, ukarimu unahesabiwa kama sifa ya muhimu sana kwa mwanamke ambaye ana kiu ya ndoa. Ukarimu ni roho nzuri, huwezi kuwa mkarimu kama huna upendo, kukiwa na upendo ndani yako, hapo ndipo utakapokuwa na ukarimu.
Ukarimu utaanzia kwa mumeo kwanza, unakuwa naye karibu kwa kila kitu, kumuandalia chakula kizuri, kumpa pole akitoka kazini na hata kuwa mshauri wake anapokuwa na matatizo.
Hata hivyo, ukarimu hauishii hapo rafiki yangu, utatakiwa kuonesha ukarimu wako hata kwa rafiki zake wa karibu, mnapotembelewa na wageni nyumbani, lazima uoneshe ukarimu wako na upendo wa hali ya juu.
Inawezekana kwasasa bado mpo katika uchumba, lakini mara nyingi umekuwa ukienda nyumbani kwake kwa ajili ya kumfanyia usafi na kazi nyingine ndogondogo, rafiki zake wanapokuja, lazima uwakarimu.
Wapokee kwa upendo, watayarishie chakula au kinywaji, fanya kila unaloweza ili ukiondoka, wamweleze rafiki yao kwamba wewe ni mwanamke mwenye upendo na ukarimu. Dada yangu, ukiwa na sifa hii, utakuwa unajiweka jirani kabisa na ndoa. Tiba ya tatizo lako, ipo mikononi mwako mwenyewe.
4. Asiyehesabu makosa
Kukosea ni sehemu ya kujifunza, lakini inashauriwa kwamba mkosaji akigundua kwamba amekosea ni vyema akaomba radhi haraka. Katika mapenzi, kukosea ni kawaida na inawezekana mpenzi wako akawa anakosea mara nyingi sana, anakuudhi mara nyingi lakini anaomba msamaha.
Kuomba msamaha ni kujishusha, muungwana pekee ndiye anayeweza kufanya hivyo. Sasa kama mwenzi wako amekuomba msamaha, jifunze kusamehe kwa moyo, ukisamehe kwa dhati huwezi kukumbuka makosa, lakini ukisamehe kinafiki ni rahisi sana kukumbuka makosa ya mwenzako. Pointi kubwa hapa ni kwamba, hata kama mpenzi wako atakuwa amekukosea mara ngapi, kamwe usimkumbushe au kumsimanga kwamba amekuwa akikosea kila wakati.
“Kila siku wewe unakosea, mwezi uliopita ulinikosea, tena ukanipeleka mpaka beach kuniomba msamaha nikakusamehe. Hatujakaa sawa, ukakosea tena, ukalia chini ya miguu yangu, nikakusamehe.
“Wiki iliyopia tena ukafanya madudu yale yale na leo umerudia, wewe ni mpenzi wa aina gani, wewe ni mwanaume gani ambaye hauna msimamo? Kwa hili leo siwezi kukusamehe, kweli sitaweza!”
Kauli kama hiyo hapo juu si nzuri kabisa kwa mpenzi wako, unajua mara nyingi maneno mengi husababishwa na hasira, ukitulia hasira ikaisha¸unagundua kwamba hukuwa sahihi kutoa maneno fulani kwa mpenzi wako. Mtayazungumza yataisha, lakini ndani yake utakuwa umemwacha na funzo la mashaka, kwamba wewe si mwanamke sahihi kwake, jambo ambalo halitakuwa zuri. Sifa yako ya kuwa mke, utakuwa umeipoteza kuanzia hapo. Hakikisha una sifa hii.
3 Msaidizi
Upo msemo wa siku hizi, unasema; “Haki sawa kwa wote!” Huu ni msemo ulioundwa maalum kwa kutetea haki za wanawake. Wanataka haki sawa. Hakuna ubaya katika hili, lakini wanaume kwa kuzingatia msemo huo, siku hizi hawataki baba awe kila kitu nyumbani, mama awe msaidizi wa kweli.
Usaidizi ninaouzungumzia hapa ni kusaidiana majukumu mbalimbali ya familia, kwakuwa bado mpo katika uchumba, hutatakiwa kuwajibika sana katika mahitaji ya nyumbani kwake, lakini angalau ukionekana unachakarika na kazi yoyote, unakuwa umeingia kwenye cheni ya kuwa msaidizi wake wa baadaye.
Usichague kazi, bora iwe halali, jishughulishe ili uonekane siyo aina ya wanawake wale wanaopenda kuitwa ‘golikipa’. Hii ni sifa muhimu sana ambayo wanaume wengi wa sasa wanapenda wanawake wawe nazo.
“Kaka siwezi kuoa mzigo, mwanamke wa maisha yangu lazima awe anajishughulisha, kama hutakuwa makini, unaweza kuoa mzigo ambao hata chumvi ikiisha nyumbani atakubeep umpigie ili akuambie eti chumvi imeisha! Huu si uzembe?!” Anasema Roges (28) mfanyakazi wa Saluni moja ya kiume, Sinza ya Mori jijini Dar es Salaam katika mahojiano maalum nami hivi karibuni.
Umeona? Hapo ni kazi kwako kubadilika na kuhakikisha unakuwa na sifa hizo. Wiki ijayo tutamalizia sifa mbili za mwisho zilizosalia. Usikose.

KUMBE DR. SLAA UMEPORA MKE WA MTU?
Mume wa ndoa wa Josephine Mushumbusi
"NAKUACHIA kibanda chako, nakwenda kwenye nyumba

Hayo yalikuwa maneno ya mwisho ambayo Aminiel Mahimbo aliambiwa na mkewe, Josephine Mushumbusi siku alipoachwa na mkewe huyo aliyeamua kwenda kwa mgombea wa urais wa Chadema, Dk. Willibrod Slaa.
Mahimbo ambaye ni mume halali wa Josephine, (kwa ndoa ya kanisani) alisema anakumbuka kuwa ilikuwa Machi mwaka huu na hakujua mke wake alipokuwa akienda na wala hakuhisi dalili yoyote ya kuwepo kwa mwanamume mwingine katika ndoa yao mpaka siku mwanawe wa kwanza Upendo (7) alipomwambia “baba tunaishi na daddy”.
Akisimulia kisa hicho kilichoanza takribani miezi saba iliyopita, katika mahojiano maalumu na gazeti hili jana, Mahimbo ambaye ndoa yake ilifungwa Agosti 16, 2002 na Mchungaji Lewis Hiza katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Kijitonyama, jijini Dar es Salaam, alisema hakujua kama huyo ‘daddy’, ni Dk. Slaa mpaka siku moja alipoambiwa na mama mkwe wake.
“Baada ya (Josephine) kuondoka nyumbani, tulikwenda mpaka nyumbani kwao kusuluhishana, lakini alikataa katakata kurudi nyumbani na wazazi walikasirika na kumfukuza.
“Siku moja mama mkwe alikuja Dar es Salaam (kutoka nyumbani kwao Mwanza) na alikwenda kumtembelea mama yangu Kijitonyama,” alisimulia.
Alisema alipopata taarifa ya kuwepo kwa mama mkwe wake Dar es Salaam, aliwasiliana naye kwa simu na katika mazungumzo hayo mama huyo alikuwa akilia huku akimwambia kuwa mume mpya ni Dk. Slaa.
“Nilimpigia baba yake mdogo, Ruhendela (hafahamu jina la pili anahisi ni Mushumbusi ambalo ni la ukoo) kutaka kufahamu ukweli wenyewe, akathibitisha hilo na kusisitiza kuwa familia haimtambui mheshimiwa, inanitambua mimi,” alisema.
Kabla ya kufahamu hilo, Mahimbo alisema siku moja ilikuwa sikukuu, akaomba kupewa watoto awapeleke kwa bibi yao, na walipokuwa njiani, mwanawe Upendo alimwonesha hoteli ambayo Josephine, Dk. Slaa na watoto hao walikuwa wakiishi.
“Sikumbuki jina, ila ipo barabarani ukishapita Makongo maeneo ya Tegeta na siku hiyo baada ya kuwarudisha watoto, mama yao aligundua Upendo katoa siri ya mahali wanapoishi.
“Alimpiga na baada ya hapo akanipigia simu na kumpa Upendo aongee na mimi, alikuwa akilia akisema baba njoo unichukue siwezi kuishi huku,” alisimulia Mahimbo.
Alisema wakati akijitayarisha kwenda kumchukua mwanawe, ndugu zake walimshauri asiende kwa kuwa ilikuwa saa tatu usiku na walikuwa wakihofia usalama wake.
Kwa mujibu wa Mahimbo, mama mkwe wake alimwambia kuwa Dk. Slaa na Josephine, walihamia katika hoteli ya Abla Hotels Apartment iliyopo Victoria Dar es Salaam.
“Nafikiri bado wapo hapo, juzi juzi nilikwenda hapo kutaka kuonana na mheshimiwa (Dk. Slaa), waliniambia kuwa yupo ndani amepumzika siwezi kumuona muda huo,” alisema Mahimbo.
Gazeti hili liliwasiliana na hoteli hiyo kwa simu ambapo mhudumu mmoja alisema hawezi kuelezea taarifa za watu, lakini akathibitisha kuwa Dk. Slaa alikuwa akiishi hapo.
Mahimbo alisema aliwasiliana na Mchungaji Hiza ambaye aliahidi kuzungumza nao tofauti kabla ya kuwaita pamoja kwa ajili ya usuluhishi.
“Nimeongea na Mchungaji Hiza, amesema ameshazungumza na Josephine na ataniita kwenda kuzungumzia hilo, juzi alikuwa Dodoma kulikuwa na mkutano wa viongozi wa dini,” alisema.
Pia Askofu Mkuu wa KKKT, Alex Malasusa alipohojiwa alisisitiza kuwa hawezi kuzungumzia hilo kwenye simu.
Hata hivyo Mahimbo alisema zamani alikuwa akizungumza na watoto wake, Upendo na Precious, lakini kwa sasa ana miezi miwili au zaidi ya mmoja tangu awaone watoto hao na hata simu siku hizi hawapewi.
Mahimbo alisema hakuwahi kuhisi kwamba mkewe alikuwa akiisaliti ndoa yao na mara kwa mara alikuwa akisafiri kwenda mikoani hasa Dodoma wakati wa Bunge akijua ni kikazi mpaka alipofahamu kuwa mkewe anaishi na Dk. Slaa, ndio aliposhituka kuwa safari za mkewe Dodoma hazikuwa za kikazi tu.
Alisema mpaka sasa Josephine ni mke wake halali, lakini hana hakika kama wanaweza kurudiana tena kwa kuwa amemdhalilisha.
Na wakati Mahimbo akiwa njia panda akishindwa kujua hatima ya ndoa yake, Dk. Slaa, Padri msomi `amelitangazia’ taifa mbele ya mikutano ya kampeni ya chama chake cha Chadema kuwa Josephine ndiye mke wake mtarajiwa.
Katika kudhihirisha kuwa `hatanii’, amekuwa akizunguka naye katika mikoa mbalimbali nchini anakopita kufanya kampeni ya kuomba ridhaa ya kuchaguliwa kuwa Rais wa Tanzania baadaye mwaka huu.
Dk. Slaa alidiriki pia kumkana mke wake wa miaka nenda miaka rudi, Rose Kamili aliyezaa naye watoto wawili, akidai kwa sasa hana mahusiano naye, bali ana `chombo kipya’, Josephine.
Ni baada ya kumtangaza Josephine ndipo habari zilipovuja kuwa, mwanamke huyo anayetamba naye Dk. Slaa ni mke wa mtu aliyefunga ndoa kanisani mwaka 2002, lakini akaamua kuondoka katika mazingira ya kutatanisha na kutua kwa mgombea huyo wa urais kwa tiketi ya Chadema.
Kwa upande wa Rose, mwanaharakati na mwanasiasa aliyeiongoza CCM katika Kata ya Basotu Hanang akiwa Diwani kwa miaka 16 kabla ya kuhamia Chadema hivi karibuni na kutangaza kugombea ubunge Hanang, amekuwa kimya kuzungumzia suala la mumewe.
Na hata juzi walipokutana katika kampeni za Dk. Slaa mkoani Manyara.
Rose ingawa alikuwa jukwaa moja na Josephine alionesha ukomavu kwa kujali kampeni zake hadi mgombea huyo wa urais alipoondoka Hanang kwenda Mbulu kuendelea na kampeni zake.
Monday, January 17, 2011
SLOW DOWN ZONE......!!!!
Hiki nikipindi ninachokiendesha mm katika kituo cha Radio Nuru fm 93.5 Mhz. kuanzia saa 4:00 mpk 7:00 usiku karibu tuwe sote.
Sunday, January 16, 2011
HUYU JAMAA AMEPOTEA KABISAAA
Baada ya kujishindia mapesa na usafiri wa uhakika moja kati ya watu waliovuma sana Jumanne Iddy na kupata tatizo la ajari ya gari hiyo jamaa ameuchuna mpaka leo.
Rita Paulsen
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni maarufu ya Benchmark Productions yenye makao yake makuu jijini Dar-es-salaam.
BAADA YA KUPIGA SHOW! KUUZA SURA KUNAFUATA.
(Kushoto) Beatrice wa BSS,Steve Magombeka (Kasampaida)PNC Mtaalaam wa kullia viburudisho baada ya kumaliza show na mradi wa vunja ukimya! Uliosababisha kutembelea mikoa yote ya Tanzania.
tarehe 17 ni birthday ya Mohamed na wife wa Obama.
Huyu ndo mke wa rais wa malekani, Rais barack Obama na leo ndio sikuya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake.ANAUMRI WAMIAKA 26
Nickname(s) | The Greatest The Champ The Louisville Lip |
---|---|
Rated at | Heavyweight |
Height | 6 ft 3 in (1.91 m) |
Reach | 80 in (203 cm) |
Nationality | ![]() |
Birth date | January 17, 1942 (1942-01-17) (age 68) |
Birth place | Louisville, Kentucky, United States |
Stance | Orthodox |
Boxing record | |
Total fights | 61 |
Wins | 56 |
Wins by KO | 37 |
Losses | 5 |
Draws | 0 |
No contests | 0 |
Muhammad Ali (born Cassius Marcellus Clay, Jr.; January 17, 1942) ANAUMRI WA MIAKA 68.
DALILI 10 ZA MWANAMKE ASIYEKUPENDA.
1 : Hataki kuambatana na wewe katika matembezi na kama ikiwa lazima anakuwa mtu wa masharti mara akuambie tangulia nakuja au kutembea nawe kwa mbali.
2: Anapata kigugumiza kukutambulisha kwa rafiki zake na jamaa zake.
3: Haonyeshi kubana matumizi kwa ajili ya maendeleo, kwake ni kufuja na kwenda mbele na huwa mfujaji mkubwa wa pesa na anapokosa kununa kabisa.
4: Anaahirisha kukutana na wewe mara kwa mara, tena bila kukueleza sababu za msingi, au kukutungia uongo wa dhahiri.
5: Anapokuwa akitoa maelezo ya mwanamme amtakaye sifa zake zinakuwa hazilingani na wewe, kwa mfano atakwambia napenda mwanamme mwenye mwili mkubwa , sifa ambazo wewe huna.
6: Hacheki kwa furaha, hata kama ukimchekesha haonyeshi furaha ya moyoni, ukimwambie twende tukatembee forodhani atakujibu ''Aaah, nimechoka mie nipo nyumbani'
7: Huwa hana wivu kabisa, hudiriki hata kukushawishi uwende Disco peke yako.
8: Hasamehe na kusahau, kosa la mwaka juzi analijengea hoja.
9: Humsisimui katika mambo ya faragha.
10: Mwepesi wa kutoa kauli ya TALAKA, ''kama vipi bora kila mtu akae kivyake vyake'' tena hataki kuambiwa ukweli na anapotokea akaambiwa hujitetea kwa kumtaja mwanaume mwingine '' Mbona Al-Udii (si jina halisi) anamfanyia hili , hamfanyii hivi mkewe''
BADO NDANI YA MATUMAINI KUWABURUZA WASHABIKI.
Beka ni msanii mwenye umri mgodo anae sifika kwa kuteka nyoyo za watu wazima kutokana na sauti pamoja na Umahiri wake wa Utunzi wa mashairi na Hivi sasa Beka anatamba na ngoma yake kali kabisa aliyo itolea remix inayoenda kwa jina la "Natumaini remix" ambayo nafanya vizuri kwa mwaka 2011.
Saturday, January 15, 2011
HIZI NI LOGO AMBAZO MIMI NINAZIKUBALI.
WATU WANAO DEAL NA BASKET HAPO MTANIELEWA.
NA HAPA MADANCER WOTE WANAJUA NINACHOMAANISHA.
OK! MADJ WOTE TUPO PAMOJAAA.....????
NA HUMU NDIPO TUNAPOPATA RADHA YA MUSIC KWA MARAPPER WOTE....
NA HAPA MADANCER WOTE WANAJUA NINACHOMAANISHA.
OK! MADJ WOTE TUPO PAMOJAAA.....????
NA HUMU NDIPO TUNAPOPATA RADHA YA MUSIC KWA MARAPPER WOTE....
PRO24DJS
Hawa ni wakali wa kuwaburudisha wale wote wapendao burudani ya music na kwasasa wameuva mia mkoa wa Iringa katika Club VIP ni noumaah!!!
Hapa ni kazi mbili kwa wakati mmoja ni noumaah!!! (kushoto) ni Dj Arnold na anayefuata ni Peter moe
Wote mnakaribishwa....!!!!!
Hapa ni kazi mbili kwa wakati mmoja ni noumaah!!! (kushoto) ni Dj Arnold na anayefuata ni Peter moe
Wote mnakaribishwa....!!!!!
TUZUNGUMZE MAPENZI!
Kila mtu anajua habari za mapenzi,hata wewe unayesoma habari hii unajua habari hizi. Mapenzi ni matunda matamu na pia ni matunda machungu.Sijui inategemea nini lakini nadhani ni kadri unavyoyapata,unavyoyala,na unavyojisikia wakati unaanza kula au unapomaliza.
Blog hii ni ya watu wazima,watu wanaojua nini maana ya mapenzi au wanaojaribu kujua zaidi.Nimeamua kuanzisha blogu hii kwa sababu najua ipo haja ya watu kuendelea kubadilishana mawazo juu ya mapenzi,ngono na mengineyo yanayohusiana na miili yetu,zikiwemo afya zetu.Si mnajua kwamba kitumbua siku hizi kimeingia mchanga ndugu zangu?
Kwa hiyo keti kitako tuanze kuyachambua masuala ya mapenzi. Kwa utaalamu wangu wa masuala haya nadhani nitakuwa tayari kujibu maswali yenu,hoja zenu nk kuhusiana na mapenzi,kujamiiana(ngono) na mengi mengineyo. Jisikie huru kunitumia email au kuuliza swali lako hapa hapa,nitakujibu. Lakini kwa kuanzisha hoja,hebu niambie,mapenzi ni nini kwa jinsi unavyoelewa wewe?Ni kwanini eti watu wanauana,wanafarakana,wanachinjana,nchi zinaingia kwenye vita kisa mapenzi? Je hayo yanabakia kuwa mapenzi au chuki? Kuna uhusiano gani kati ya mapenzi na wivu?Yupi ana nguvu kumshinda mwenzake?
NDIO KWANZA TUNAUANZA MWAKA.
Watu 4 wamekufa,8 wamejeruhiwa baada ya lori lililokuwa linaenda Zambia kugonga Hiace huko Tanangozi nje ya Iringa.
KARIBUNI JAMANI......!!!
HUU NIMWAKA MPYA JAMANI NA HII NI BLOG MPYA AMBAYO NINAWAKARIBISHA WADAU WOTE TUWEZE KUSHIRIKIANA KWA PAMOJA HUU NIMWAZO BADO NAKARIBISHA MAONI YAKO MDAU
Subscribe to:
Posts (Atom)