Sunday, January 16, 2011

DALILI 10 ZA MWANAMKE ASIYEKUPENDA.


1 : Hataki kuambatana na wewe katika matembezi na kama ikiwa lazima anakuwa mtu wa masharti mara akuambie tangulia nakuja au kutembea nawe kwa mbali.

2:  Anapata kigugumiza kukutambulisha kwa rafiki zake na jamaa zake.

3:  Haonyeshi kubana matumizi kwa ajili ya maendeleo, kwake ni kufuja na kwenda mbele na huwa mfujaji mkubwa wa pesa na anapokosa kununa kabisa.

4:  Anaahirisha kukutana na wewe mara kwa mara, tena bila kukueleza sababu za msingi, au kukutungia uongo wa dhahiri.

5:  Anapokuwa akitoa maelezo ya mwanamme amtakaye sifa zake zinakuwa hazilingani na wewe, kwa mfano atakwambia napenda mwanamme mwenye mwili mkubwa , sifa ambazo wewe huna.

6:  Hacheki kwa furaha, hata kama ukimchekesha haonyeshi furaha ya moyoni, ukimwambie twende tukatembee forodhani atakujibu ''Aaah, nimechoka mie nipo nyumbani'

7:  Huwa hana wivu kabisa, hudiriki hata kukushawishi uwende Disco peke yako.

8:  Hasamehe na kusahau, kosa la mwaka juzi analijengea hoja.

9:  Humsisimui katika mambo ya faragha.

10: Mwepesi wa kutoa kauli ya TALAKA, ''kama vipi bora kila mtu akae kivyake vyake''  tena hataki kuambiwa ukweli  na anapotokea akaambiwa hujitetea  kwa kumtaja mwanaume mwingine '' Mbona Al-Udii (si jina halisi) anamfanyia hili , hamfanyii hivi mkewe''

No comments:

Post a Comment