Wednesday, August 10, 2011

Safari yangu ya Dar! (picture)

Jamaa huyu nimemkuta amelala maeneo ya Round about ya shule ya Uhuru akiwa amelala mida ya saa 12:45 mchana huku akiwa haelewi kinachoendelea wala kugundua kama kumekucha. Jengo unaloliona hapo juu ni ngao kubwa na yenye kuonyesha saa ya jiji kwa maeneo hayo ya njia panda ya kuelekea Kamata,Kariakoo Mnazi mmoja,Muhimbili, na Karume. Jamani vijana tukomaeni katika kujishughulisha na kazi mbali mbali ili kuepuka haya mazingira ya namna hii.
Jamani hapo ni maeneo ya Kigamboni nimji wenye sifa ya peke yake na kama unavyojionea huyo nao ni moja ya vijana wanaopenda kujishughulisha na biashara na hapo anauza hao ni samaki aina tofauti kidogo na wengi hupendelea kuwaita Pweza na hapo wapo mchanganyiko na dagaa kamba. wanaouzwa kwa vipande na watuwengi wakiwa wanapendelea kupata burudani ya samaki hao

No comments:

Post a Comment