Thursday, July 21, 2011

Moto umewaka mkoani Mkoani Iringa.

Wadau Usiku wa kuamkia leo Moto umewaka na kuleta hasara kubwa  kwa wafanya biashara na wakazi wa maeneo ya Kihesa sokoni katika halmashauri ya mkoa wa Iringa, Na baada ya kufika kikosi cha kuzima moto eneo hilo nakufanikiwa kuzima moto huo bila yakuweza kuokoa mali za wahusika hao walipo ondoka tu! eneo la tukio ghafla moto ukaanza eneo lingine kando kigodo na mahali hapo.
Hili ndilo eneo lililoathirika na moto huo.
Baada ya kikosi cha kuzima moto kuzima moto eneo lile na kuondoka nyumba hii unayoiona hapo ndipo ilipoanza kuungua ambapo kwa mujibu wa maelezo ya wahusika inasemekana kuwa moto huo ulisababishwa na Mshumaa.
HUmu ndio ndani ya chumba kilichokuwa kimewaka moto kunateketeza baadhi ya vitu kutokana na mshumaa.
Huyu ni mmiliki wa nyumba hiyo iliyokuwa imewaka moto hapa akikakugua baadhi ya vitu na kuangalia usalama usiku huo baada ya janga hilo kutokea.

No comments:

Post a Comment