Sunday, July 31, 2011

Matokeo ya Miss Ilala 2011


 
Aliyekuwa akisakwa kwa udi na uvumba kwenye kitongozi cha Ilala sasa apatikana, si mwingine bali ni Mlimbwende Salha Israel ( Miss Ilala).

Mlimbwende huyo hakuwa mwenyewe bali aliambatana na washindi wa pili na watatu, akiwemo Alexia William na Jenifer Kakolaki waliojinyakulia tiketi ya kushiriki shindano la kifaifa la Vodacom Miss Tanzania 2011.

Ushindi huo mnono wa mwanadada huyo ambaye kwa sasa ndiye Miss Ilala, ulipatikana usiku wa kuamkia jana ndani ya Viwanja vya Mnazi Mmoja hapa Jijini.

No comments:

Post a Comment