Thursday, July 28, 2011

SAKATA LA SAMAKI WA SUMU NANI ALAUMIWE?


SAKATA la samaki wanaodaiwa kuwa na sumu kutoka Japan walioingizwa nchini, limefikishwa bungeni na wabunge wameitaka Serikali ifafanue ukweli wa jambo hilo ikiwa ni pamoja na kueleza ni namna gani waliingizwa.

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji, Kambi ya Upinzani pamoja na wabunge waliochangia jana bungeni kwa nyakati tofauti, walieleza kushitushwa na taarifa hizo na wakataka Serikali itoe tamko bungeni.

“Kuna taarifa kwamba samaki wenye sumu wameingizwa nchini, pamoja na uzito wa jambo hili, Serikali haijatoa tamko. Kwa mamlaka niliyo ayo, naitaka Serikali itoe tamko ieleze ukweli wa suala hili na hatua zinazochukuliwa,” alisema Mbunge wa Sikonge, Said Nkumba (CCM) kwa niaba ya Mwenyekiti wa Kamati, Profesa David Mwakyusa.

Mbunge huyo alikuwa akisoma taarifa ya Kamati ya Bunge kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi na Makadirio ya Matumizi ya mwaka 2011/12.

Kambi ya upinzani kupitia kwa Msemaji wake Mkuu kwa Wizara ya Maendeleo na Mifugo, Silvester Kasulumbayi, ikitumia taarifa za vyombo vya habari vya Julai 26, ilihoji ni namna gani kampuni ya Alphakrust Limited ya Dar es Salaam, iliruhusiwa kuingiza samaki hao.

“Kama TDFA ndiyo waliotoa kibali cha kuingizwa kwa samaki hao baada ya kufanya ukaguzi na kujiridhisha kuwa hawana madhara, ni nani na wa mamlaka gani aliyegundua kuwa wana madhara? Ni hatua gani zimechukuliwa dhidi ya maofisa waliohusika kutoa kibali husika?” alihoji Kasulumbayi.

Wabunge hao wa upinzani walihoji sababu ya Tanzania yenye maziwa na bahari kuagiza samaki kutoka nje ya nchi. “Kwa rasilimali hii yote tuliyopewa na Mwenyezi Mungu iliyojaa samaki wengi wa kila aina, kama Taifa tuna haja kweli ya kuagiza samaki kutoka nje ya nchi?
“Kwa nini fedha zetu za kigeni zisitumike kununua mahitaji mengine ambayo hayapatikani nchini?” aliendelea kuhoji.
Wakati huo  ni wazi kabisa tunakumbuka Serikali ilipokuwa imefungia biashara ya Kuuza nyama ya nguruwe kwa kusababu walizosema kuwa Ni Uchafu kwa watu ambao wanaandaa nyama hizo.

No comments:

Post a Comment