Tuesday, July 12, 2011

Biashara kwa watoto.

Kijana huyu nilikutana nae jana! nikiwa kwenye matembezi yangu ndipo nilipopata nafasi yakuzungumza nae nakujaribu kudodoso habari na vitu vinavyomhusu kijana huyu (ambaye jina lake nimeliifadhi) kutokana na umri wake ambao kwa sasa ni miaka(16) anajishughulisha na biashara ya kuuza mayai ya kuchemsha nakujitegemea kimaisha pamoja na kuisaidia Familia yake kwa namna moja ama nyingine kwa kuchangia fedha kidogo kwa matumizi ya kifamilia, mahali anapoishi ni Kiodombi wilaya ya Iringa mjini mkoani Iringa. Hapa akionekana yupo tayari kuondoka kwenda kufanya biashara yake ya kuuza mayai mitaani na toka aanze biashara hiyo sasa ni zaidi ya miaka minne (4).
  Hapa akiwa na mwenzake ambaye naye anajishughulisha na uuzaji wa mayai Mkoani Iringa wakiwa wanaoneka ni watu wa furaha wakijaribu kunionyesha baadhi ya vituko ikiwa ni pamoja na kustua kijiti, tayari kwa kwenda kwenye shughuli zao.
Hapa ndio nlipoweza kuonana nae akiwa amefika sehemu ambayo huwa anaenda kula akiwa na Rafiki yake huyo ambaye wanafanya wote biashara hiyo ya kuuza mayai.

No comments:

Post a Comment