Tuesday, February 15, 2011

Nini ukweli kuhusu Jay Z na ibada za kichawi?


jay-z-1
Rapa maarufu na mmiliki wa lebo ya Roca Fella, Shawn Carter ‘Jay Z’,amekana kuwa mwanachama wa makundi ya imani za giza ya Illuminati na Free Mason yanayohusishwa na kuendesha imani za kishetani.
Licha ya kukana, Jay Z amefanya kolabo na Rick Ross katika ngoma waliyoipa jina la ‘Free Mason” inayopatikana katika albamu  mpya ya Rick Ross, Teflon Don. Mashairi yanayopatikana katika wimbo huo yana maelezo mengi kuhusu Illuminati,Free Mason na Lucifer,hali inayotafsiriwa kuwa Jay Z ana ufahamu mkubwa katika nguvu za giza, na huenda ni mwanachama ingawa  mwenyewe hataki kukiri.
Jay Z amekuwa akihusishwa kuwa mwanachama wa makundi hayo kutokana na mazoea yake ya kutumia alama zinazotumiwa na Illuminati na Free Mason,kama kunyoosha vidole viwili hewani, na nembo za Illuminati na Free Mason katika maonesho yake mengi ya muziki na kwenye albamu zake.

No comments:

Post a Comment