Sunday, July 31, 2011

Big Brother Amplified Winners Are Karen and Wendall



This years season of Big brother came to an end on Sunday with Nigeria's Karen and Zimbabwe's Wendall taking the money. We had seven finalists who were reduced to the top five after Vina from Nigeria and Hanni from Ethiopia were evicted in that order.
IK bounced back to the house and called Lomwe, Wendall, Luclay, Sharon and Karen to leave the house. Now these were the top five but with Karen's name being called out last, she thought they were leaving her behind and as usual she had started with her noise drama.
While the top five were on stage, IK kept on interviewing one by one but when it got to our very own Sharon, they asked her about Michael, to which she said that Michael was like a brother to her before shouting that "Michael from Mozambique, you got the swagg." She then told IK of how she was going to win.
Unfortunately for Sharon O, then next time IK called the housemate to be evicted, it was Sharon O who almost failed to walk from where she was seated to IK, the host of the show. IK told her that at least she had beaten all the housemates who were before her, but that did not seem like what she had wanted.
Of the top five, Sharon had been evicted leaving four housemates, Karen, Wendall, Luclay and Lomwe. IK called out Lomwe next leaving the big three. Many had thought Luclay and Karen were winning and to some, they thought the next name to be called was Wendall but no please, IK called Luclay.
The crowd started making some sounds as if to suggest there was some unfairness, but this was Africa's decision at work. Otono was dressed like a gangsta prompting a huge statement from IK that; "I have never seen anyone dress like that for this show."
He quickly told him it was his job to tell Africa who is next to leave the house but before that , he reminded him of the scratch on his chest, that never was and yet made him and Karen spit fire in the house, you have been evicted.







Zimbabwe surprised the entire Africa when the pilot was one of the winners and Karen, much as she played the game so well, she was one of the predictable winners and took the money anyway, it is the third time Nigeria is taking the moola after Kevin and Uti from Nigeria won the previous shows.
It's been nice hosting you this season, catch you on the next version.

Matokeo ya Miss Ilala 2011


 
Aliyekuwa akisakwa kwa udi na uvumba kwenye kitongozi cha Ilala sasa apatikana, si mwingine bali ni Mlimbwende Salha Israel ( Miss Ilala).

Mlimbwende huyo hakuwa mwenyewe bali aliambatana na washindi wa pili na watatu, akiwemo Alexia William na Jenifer Kakolaki waliojinyakulia tiketi ya kushiriki shindano la kifaifa la Vodacom Miss Tanzania 2011.

Ushindi huo mnono wa mwanadada huyo ambaye kwa sasa ndiye Miss Ilala, ulipatikana usiku wa kuamkia jana ndani ya Viwanja vya Mnazi Mmoja hapa Jijini.

Saturday, July 30, 2011

Kesi mpaka Muhimbili.


HOSPITALI ya Taifa ya Muhimbili (MNH), imegeuka kuwa mahakama kwa muda baada ya dereva wa Kampuni ya Mabasi ya Hood Ltd, Saleh Tembo (42), kusomewa mashtaka 23, chini ya ulinzi kwenye hospitali hiyo.
Tembo anadaiwa kusababisha ajali hivi karibuni iliyopoteza maisha ya watu sita na wengine 17, kujeruhiwa amelazwa wodi namba 17 Sewahaji kwa matibabu, baada ya kuvunjika mguu na mbavu.


Katika ajali hiyo, basi hilo liligongana na lori la mafuta na kusababisha magari yote kuteketea kwa moto.
Dereva huyo alisomewa mashtaka akiwa chini ya ulinzi wa polisi, anadaiwa kusababisha vifo vya watu sita barabara ya umma na kuendesha gari kwa mwendokasi na kusababisha abiria 17 kujeruhiwa.

Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Naima Mwanga, alidai mshtakiwa alitenda makosa hayo Julai 20, mwaka huu barabara ya Morogoro-Iringa , kwenye Hifadhi ya Taifa Mikumi, Wilaya ya Kilosa.

Mwanga alidai siku ya tukio saa 11:30 jioni katika hifadhi hiyo, akiwa dereva wa basi la Hood aina ya Scania, mshtakiwa anadaiwa kuendesha gari kwa uzembe na kugonga gari aina ya Semi Trela, mali ya Kampuni ya Frank Kefa, kisha kusababisha kifo cha dereva wa lori hilo, Bure Mayenga.

Shtaka la pili, anadaiwa kuua dereva msaidizi wa lori, Frank Kefa, ambaye ni mmiliki wa kampuni ya magari hayo.
Shtaka la tatu, siku na wakati huohuo anadaiwa kumuua kondakta wa basi hilo, Ibrahimu Shitindi, wakati shtaka la nne anadaiwa kumuua abiria wa basi, Joyce Kanikanila.

Mwanga alidai shtaka la tano, mshtakiwa anadaiwa kuumua abiria mwingine ambaye hakutambulika kutokana na kuungua na kubaki majivu. Shtaka la sita, anadaiwa kujeruhi James Shitindi, Peter Jamino, Elina Malekela na Joranda Mwasifiga.

Aliendelea kudai kuwa, mshtakiwa akiwa dereva wa mabasi ya Hood na mkazi wa Mbezi, alisababisha majeruhi kwa kuendesha gari kwa uzembe na hatari, ambao ni Leila Mgimwa, Amrani Salehe, Beatrice Mofuta, Rose Zambi, Jemina Ayuob na Richard Lubuvu.

Wengine waliojeruhiwa ni Theodory Raphael, Evance Mwasifiga, Benito Suga, Milk Maneno, Narropil Siroia, Kissa Mwakabuga, Asha Maneno na Charles Yesaya.Mtuhumiwa alikana kuhusika na tukio hilo na hakimu Janeth Kaluyenda, aliahirisha kesi hiyo hadi Agosti 10, mwaka huu itakapotajwa tena.

Kaluyenda aliahirisha kesi hiyo kutokana na mshtakiwa kusubiri kupelekwa Morogoro ili kufunguliwa mashtaka upya.

Thursday, July 28, 2011

Unatambua sifa ya wabunge waliotolewa Bungeni jana?

  
Mwanasheria Mkongwe na Machachri nchini na Mbunge (Chadema)Mheshimiwa Tundu Lissu.

Hayo ni baadhi ya Matukio na video zinazoonyesha Mh: Tundu Lisu akiwa Bungeni.
Mchangji Petwr George Msigwa ambaye nae alitolewa kwenye kikao hicho cha bunge kwa lile lililosemekana kuwa ni kutokuwa na nidhamu na kudiliki kuwasa kinasa sauti pasipo na kibali toka kwa mwenye kiti wa bunge

Wewe ni wangu kufa na kuzikana.

SAKATA LA SAMAKI WA SUMU NANI ALAUMIWE?


SAKATA la samaki wanaodaiwa kuwa na sumu kutoka Japan walioingizwa nchini, limefikishwa bungeni na wabunge wameitaka Serikali ifafanue ukweli wa jambo hilo ikiwa ni pamoja na kueleza ni namna gani waliingizwa.

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji, Kambi ya Upinzani pamoja na wabunge waliochangia jana bungeni kwa nyakati tofauti, walieleza kushitushwa na taarifa hizo na wakataka Serikali itoe tamko bungeni.

“Kuna taarifa kwamba samaki wenye sumu wameingizwa nchini, pamoja na uzito wa jambo hili, Serikali haijatoa tamko. Kwa mamlaka niliyo ayo, naitaka Serikali itoe tamko ieleze ukweli wa suala hili na hatua zinazochukuliwa,” alisema Mbunge wa Sikonge, Said Nkumba (CCM) kwa niaba ya Mwenyekiti wa Kamati, Profesa David Mwakyusa.

Mbunge huyo alikuwa akisoma taarifa ya Kamati ya Bunge kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi na Makadirio ya Matumizi ya mwaka 2011/12.

Kambi ya upinzani kupitia kwa Msemaji wake Mkuu kwa Wizara ya Maendeleo na Mifugo, Silvester Kasulumbayi, ikitumia taarifa za vyombo vya habari vya Julai 26, ilihoji ni namna gani kampuni ya Alphakrust Limited ya Dar es Salaam, iliruhusiwa kuingiza samaki hao.

“Kama TDFA ndiyo waliotoa kibali cha kuingizwa kwa samaki hao baada ya kufanya ukaguzi na kujiridhisha kuwa hawana madhara, ni nani na wa mamlaka gani aliyegundua kuwa wana madhara? Ni hatua gani zimechukuliwa dhidi ya maofisa waliohusika kutoa kibali husika?” alihoji Kasulumbayi.

Wabunge hao wa upinzani walihoji sababu ya Tanzania yenye maziwa na bahari kuagiza samaki kutoka nje ya nchi. “Kwa rasilimali hii yote tuliyopewa na Mwenyezi Mungu iliyojaa samaki wengi wa kila aina, kama Taifa tuna haja kweli ya kuagiza samaki kutoka nje ya nchi?
“Kwa nini fedha zetu za kigeni zisitumike kununua mahitaji mengine ambayo hayapatikani nchini?” aliendelea kuhoji.
Wakati huo  ni wazi kabisa tunakumbuka Serikali ilipokuwa imefungia biashara ya Kuuza nyama ya nguruwe kwa kusababu walizosema kuwa Ni Uchafu kwa watu ambao wanaandaa nyama hizo.

Tuesday, July 26, 2011

TUMEINGILIWA JAMANI!

Nikawaida ya watu wengi sikuza week end hupendelea kwenda kutembelea sehem mbali mbali za burudani kuweza kujiburudisha na kubadilishana mawazo pamoja na marafiki zao sasa kwa week hii watu wengi wamejikuta wamekusanyia Clib V.I.P katika Usiku wa Burudani Ili kufurahi na kifanya week end yao iwe poa.
Ndipo kilipotokea kituko hiki ambacho hakika ctawahi kukisahahu ni utaratibu wa kawaida wa Club hile kama mtu umefurahishwa na burudani waweza kujiunga na wenzio katika staili moja ilikufurahi zaidi, ndipo alipojitokeza jamaa ambaye Bongo120 hakuweza kutambua jina la jamaa huyo mara moja, nakuonekana akivua chasti lake ili kupata kuonekana zaidi kuliko wote waliokuwa nadi ya club hiyo.
Hapa jamaa huyo akionekana kufurahi na kujiunga na wenzie ndani ya Club V.I.P

 Hapa jamaa huyo akionekana kwambwembwe akigeuka huku na huko ili kunogesha staili yake akifatana na wadau wengine katika kucheza nyimbo za South ambazo nimara nyingi wa2 wengi huonekana wakipendelea kucheza kwa staili moja katika Club nyingi Tanzania.
Baadhi wa wadau wengine kwenye picha wakiendelea kusakata burudani Club V.I.P Iringa
 

Monday, July 25, 2011

POLISI JAMII.

Anayeonekana hapo juu kwenye picha ni AFISA MNADHIMU POLISI JAMII MKOA WA IRINGA Bw: Bundara Musiba ikiwa ndani ya studio za Nuru fm asubuhi ya leo kwenye kipindi cha Sunrise Power akijaribu kuelezea Jamii na wasikilizaji wa Radio jinsi ya kuiheshimu Sheria ya Tanzania katika lile lililoitwa UTII BILA SHURUTI ikiwa ni moja ya mikakati iliyoanzishwa mkoani Arusha kwa kuwataka wana Inchi wa tanzania kufuata sheria na taratibu za kijamii.
Hapa Bw: Bundara Musiba akijibu maswali ya wasikilizaji wa Radio Nuru fm mkoani Iringa, nakutoa maelekeza na namna ambavyo Sheria inasema na kusisitiza kuhusu Utekelezaji wa mikakati hiyo ya Polisi kwa jamii na wakazi wa mkoa wa Iringa. 

Haya ndio matokeo ya Pombe jamani.


Hili ni pozi la bwana huju ambae jina cjulipata mara moja nikiwa nimemkuta amelala barabarani baada ya kulewa mchana na kushindwa kuondoka eneo hilo sasa jamani kwa tukio kama hili kweli mtu anaweza kukushawishi kutumia Pombe ikiwa hakuna faida zaidi ya kudhalilika?

KARIBU RUAHA NATIONAL PARK (iRINGA)

Moja kati ya vitu ambavyo wakazi na wenyeji wa Iringa hujivunia ni kuwapo kwa Hifadhi hii ya taifa Inayofahamika kama RUAHA NATIONAL PARK Jina na sifa ya Hifadhi hii ni kutokana na kupitiwa kwa mto Ruaaha pamoja na bonde la Eneo hilo, Kumekuwa na wanyama wa kila aina katika hifadhi ya Ruaha pamoja na kuwa na sifa yakupokea wageni toka nchi nyingi Duniani kwa kuja kujionea maajabu ya Hifadhi hiyo ya RUAHA.
Eneo hili limetengwa maalum kwa ajili ya wageni wanaotembelea RUAHA ilikuweza kupumzika na kufurahia safari yao ikiwa ni pamoja na kutatiwa Huduma ya chakula Kizuri kinachotengenezwa hapo hapo, Malazi bora na usalama wako na mali zako hapo huzingatiwa kwa makini unapofika RUAHA NATIONAL PARK.
Huyu ni moja kati ya wamnaya wanaopatikana katika hifadhi hii ya RUAHA. anaitwa Simba akiwa amepumzika kwenye hifadhi hiyo ya Taifa.
KWA MAWASILIANO ZAIDI TEMBELEA MTANDAO WAO AU PIGA SIMU ZILIZOPO KWENYE IYO PICHA ILIYOPO HAPO JUU. WOTE MNAKARIBISHWA.....!!!

Sunday, July 24, 2011

Jebby amejikita kwenye Intrepreneurship.

Msanii wa Tanzania mimbaji na mtunzi wa muziki wa Bongo flava Jebby a.k.a kijukuu ameamua kujikita kwenye ujasiliamali Mkoani Iringa kwa kufungua Duka la Nguo la Aina zote maeneo ya Samora mkoani hapo.
Hapa Jebby (kushoto)akiwa na Mshkaji wake Ayoub nje ya duka hilo la Jebby Latest Wear wakiwa kwenye mazungu mzo wakati nikifanya mahojiano naye nyakati za jioni siku ya Ijumaa.
wakati ukafika nami nikauza nyago kama kawa ila kwa maelezo yake Jebby ilikuwa kama ifiatavyo:
"Kwanza namshkuru Mwenyezi Mungu aliye nifanya kufikia hapa na wazazi wangu bila kuwasahau mashabiki wangu, kiukweli nimefurahia mji wa Iringa hasa hii hali ya hewa....!!!
Ninawakaribisha sana watu wote kuja kupata mavazi kwa bei nafuu na yenye ubora na yanayoendana na wakati yangu ni hayo tu. 

Saturday, July 23, 2011

week end hii ndani ya Club V.I.P

Dj Pirol on the 1&2 akifanya mambo yanayo wachizisha wadau wa Burudani ndani ya club V.I.P jana usiku.
Mpango mzima wa Burudani ulisimamiwa na Matonya na alitishaaa ile mbaya jombaaaa.!
Tonya!
Dj Joe,Bony Slay na Dj Pirol.
Eddo Bashiri kama anavyotambulika ni Radio presenter wa Ebony Fm akiskilizia mchakato unavyoenda usiku huo wa Burudani ndani ya club V.I.P
Abba Ngilangwa na Mr Chakudika ndani ya V.I.P
Athumani Mwalubadu ktk pozi.

Mzuka wamashabiki.

Baba mwenye nyumba afariki Dunia.

Jamani kama mnavyoweza faham kuwa hapa duniani hakuna atakaye dumu hii nimoja kati ya matukio yanayosikitisha na yasiyozoeleka katika jamiii yetu hususani kwa sisi waTanzania hapo unapojionea kwenye picha nileo mchana tulipokuwa tuna mzika Marehem Mr Omari (ambaye alikuwa ni baba mwenye nyumba wangu) katika maeneo ya Mlolo katika manispaa ya Iringa. Mungu ailaze roho ya marehem Peponi Milele Amina.
hapa ni katika hatua ya mwisho ya tukio hilo a maziko ya Mr Omar.

Friday, July 22, 2011

Baada ya Afande kushuka jukwaa lavunjika.

Hapa show ikiwa inaendelea chini ya udhamini mkubwa wa kampuni ya SBC LTD
Wakati wa Cyrily ukafika akakamua kama kawaida.
Cyrily akishuka baada ya kumaliza show!
Afande a.k.a Mfalme akiwa back stage kuelekea on the stage.
Afande on the stage akiwaburudisha mashabiki wake.
  Afande akishuka kwenye Stage hiyo. 
Mambo yakawa hivi kama unavyojionea na Baadhi ya speeker zilizokuwa juu ya jukwaa hilo kuanguka chini kwa kile kilichosemekana kuwa Jukwaa hilo halikuwa imara kwa shughuli iliyopangiwa.

Niwakati wa wanachuo ku beng!!!!

Mambo yote nikuanzia leo usikose!!

Thursday, July 21, 2011

Moto umewaka mkoani Mkoani Iringa.

Wadau Usiku wa kuamkia leo Moto umewaka na kuleta hasara kubwa  kwa wafanya biashara na wakazi wa maeneo ya Kihesa sokoni katika halmashauri ya mkoa wa Iringa, Na baada ya kufika kikosi cha kuzima moto eneo hilo nakufanikiwa kuzima moto huo bila yakuweza kuokoa mali za wahusika hao walipo ondoka tu! eneo la tukio ghafla moto ukaanza eneo lingine kando kigodo na mahali hapo.
Hili ndilo eneo lililoathirika na moto huo.
Baada ya kikosi cha kuzima moto kuzima moto eneo lile na kuondoka nyumba hii unayoiona hapo ndipo ilipoanza kuungua ambapo kwa mujibu wa maelezo ya wahusika inasemekana kuwa moto huo ulisababishwa na Mshumaa.
HUmu ndio ndani ya chumba kilichokuwa kimewaka moto kunateketeza baadhi ya vitu kutokana na mshumaa.
Huyu ni mmiliki wa nyumba hiyo iliyokuwa imewaka moto hapa akikakugua baadhi ya vitu na kuangalia usalama usiku huo baada ya janga hilo kutokea.

Huyu ndio usher raymond wa Tanzania.

Jamaa anaitwa Aristide Rubeya ni moja kati ya jamaa wanaosemekana kuwa amefanana na Usher Raymond kwa kuonekano wa Sura.
na huyu ndio Usher Raymond mwana mziki wa Marekeni na Dencer wa miondoko ya Pop
 Hapa Aristide akiwa kwenye pozi.
 Hapa Aristide akiwa na ma fans kwenye Birthday ya  Gadner Dibibi Dar-es-salaam.
usher raymond and justin bieber