Wednesday, February 16, 2011

uwongo mwingine bana...!!!

SUGU ATEULIWA KUWA WAZIRI KIVULI WA HABARI MICHEZO NA UTAMADINI

Msanii mkongwe wa Hip-Hop toka Tanzania ,Mwanaharakati na Mbunge wa Mbeya-Mjini (CHADEMA) asiyependa kuitwa mheshimiwa,Joseph Osmond Mbilinyi aka Sugu  ameteuliwa na Kiongozi wa upinzani bungeni,Mh Freeman Aikaeli Mbowe (Mbunge wa Hai) kuwa Waziri kivuli aka Shadow Minister wa Habari,Michezo na Vijana,kwenye Bunge la Kumi linaloendelea mkoani Dodoma. Waziri Original wa Habari,Michezo na Vijana ni Mh William Nchimbi..

Tuesday, February 15, 2011

Michelle Obama Awapiga Marufuku Binti Zake Kutumia Facebook



Mke wa rais wa Marekani, Michelle Obama amewapiga marufuku binti zake kujiunga na mtandao wa Facebook. Pamoja na kwamba mke wa rais wa Marekani, Michelle Obama amekuwa akisema kuwa anataka watoto wake waishi maisha ya kawaida kama watoto wengine, amewapiga marufuku watoto wake kujiunga na mtandao wa Facebook.

Akiongea kwenye kipindi cha televisheni cha Today show, ambacho alialikwa ili kuzungumzia kampeni yake ya kuwashawishi vijana kula vyema na kufanya mazoezi, Michelle Obama alijikuta akiulizwa maswali mengi kuhusiana na familia yake.

"Mimi sipendelei watoto kujiunga na mtandao wa Facebook, sio kitu wanachokitaji kwa wakati huu", alisema bi Obama.

Michelle Obama alisema kuwa hatawaruhusu watoto wake Sasha mwenye miaka 9 na Malia mwenye miaka 12, wajiunge na mtandao huo unaoziunganisha jamii mbalimbali duniani.

Aliongeza kuwa kwa kutegemea na umri wao na muda ambao Obama atakuwa madarakani kama ni miaka miwili ijayo au sita ijayo, asingependelea kuwaona binti zake wakijiunga na mtandao huo.

Hata hivyo bi Obama hakuelezea kama uamuzi wake huo unatokana na wasiwasi wa baadhi ya watu kuhusiana na watoto kujiunga na mtandao wa Facebook ambao una jumla ya wanachama milioni 600 duniani.

Nini ukweli kuhusu Jay Z na ibada za kichawi?


jay-z-1
Rapa maarufu na mmiliki wa lebo ya Roca Fella, Shawn Carter ‘Jay Z’,amekana kuwa mwanachama wa makundi ya imani za giza ya Illuminati na Free Mason yanayohusishwa na kuendesha imani za kishetani.
Licha ya kukana, Jay Z amefanya kolabo na Rick Ross katika ngoma waliyoipa jina la ‘Free Mason” inayopatikana katika albamu  mpya ya Rick Ross, Teflon Don. Mashairi yanayopatikana katika wimbo huo yana maelezo mengi kuhusu Illuminati,Free Mason na Lucifer,hali inayotafsiriwa kuwa Jay Z ana ufahamu mkubwa katika nguvu za giza, na huenda ni mwanachama ingawa  mwenyewe hataki kukiri.
Jay Z amekuwa akihusishwa kuwa mwanachama wa makundi hayo kutokana na mazoea yake ya kutumia alama zinazotumiwa na Illuminati na Free Mason,kama kunyoosha vidole viwili hewani, na nembo za Illuminati na Free Mason katika maonesho yake mengi ya muziki na kwenye albamu zake.

Monday, February 14, 2011

Ndo tatizo la vijana! wameshaanza kuchonga mdomo bungeni.

Kiongozi wa upinzani Bungeni, Freeman Mbowe amesema ataunda baraza za Mawaziri kivuli litakalojumuisha wabunge wa Chadema pekee.

Akizungumza ofisini kwake jana, Mbowe alisema atatangaza baraza hilo wiki ijayo huku akifafanua kuwa itakuwa unafiki kwake kuunda baraza kivuli la mseto katika kipindi ambapo kuna kejeli na matusi miongoni mwa vyama vya
upinzani.

"Majeraha yote haya ni mengi, yanahitaji muda kupona, katika hatua ya sasa nitaunda Baraza la Mawaziri Kivuli
ambalo litakuwa la Chadema pekee," alisema Mbowe.

Alifafanua kuwa muda huo aliosema ni wa kutibu majeraha, ni fursa ya kuona maendeleo ya vyama vingine tofauti na Chadema katika utendaji ili kutibu na kuondoa tofauti baina yao.

Hata hivyo alisema kama ilivyo Bunge hudumu miaka mitano na Baraza la Mawaziri Kivuli pia hudumu miaka
mitano hivyo linaweza kubadilika.

"Ni matumaini yangu tutatibu majeraha yetu, kupata amani na kuwaingiza wenzetu katika Baraza la Mawaziri Kivuli. Tupende, tusipende tuna mawasiliano ya kibunge, pengine tutagundua tuna makosa au wenzetu watagundua wao walikosea, msimamo wetu ni ule ule kwa kanuni ile iliyobadilishwa, lakini sifungi uwezekano wa kuunda baraza
la mawaziri shirikishi," alisema Mbowe.

Mbowe ambaye ni mbunge wa Hai mkoani Kilimanjaro alisema kuwa anaamini busara zitarejea kwa vyama vya
upinzani na matendo yataashiria utulivu utakaowawezesha kurekebisha tofauti zao.

Akizungumzia kuchelewa kuunda baraza hilo kivuli, Mbowe alisema ni kutokana na sintofahamu utaratibu utakaotumika
kuunda baraza hilo, kutokuwepo kwa kamati za kibunge za kisekta na kwamba yupo katika hatua za mwisho kukamilisha hilo kabla ya kulitangaza wiki ijayo.

Katika hatua nyingine Mbowe alisema Chadema inaheshimu na itawapa ushirikiano wabunge wa upinzani
waliochaguliwa kuwa wenyeviti wa kamati za Bunge.

"Kuna mambo matatu yaliyopo nataka niweke wazi, kanuni tayari, chaguzi za kamati tayari, binafsi naheshimu wabunge wenzangu, wote wana uwezo mzuri. Naheshimu waliochaguliwa uenyeviti wa kamati walio upande wa CCM hata upinzani, Chadema tutawapa ushirikiano kipekee walio nje ya CCM," alisema Mbowe na kuongeza:

"Tutawasaidia kwa kila linalowezekana, pamoja na kuwa tulitofautiana na bado tunatofautiana kuhusu kanuni, wana jukumu kubwa kwa Watanzania, tutwasaidia, Cheyo, Mrema na Zitto waweze kufanya kazi kwa ufanisi."


Alisema kimsingi Zitto, Cheyo na Mrema wanatakiwa kuwa polisi kwa CCM na serikali, lakini bahati mbaya wapinzani wamewapa CCM fursa ya kutekeleza mkakati wa kuwagawa na kuwatawala na wamefanikiwa azma hiyo.

Awali Mbowe alieleza kuwa tangu kampeni hata baada ya uchaguzi kumekuwa na hali ya sitofahamu baina ya vyama vya upinzani hali iliyoutikisa upinzani.

Alisema hali hiyo ya wapinzani kutetereka, imeipa CCM nguvu ya kuwa 'broker' (dalali) wa kuwachagulia namna ya kufanya mambo yao.

"Katika mtiririko huo, tumeifanya CCM broker, broker anapokuwa adui yenu atawapa mkakati wa kuwekana sawa
ili mumkosoe?," alihoji.

Wednesday, February 9, 2011

Twanga Pepeta waandaa varangati Valentine`s Day Tabata

Bendi ya African Stars maarufu kama Twanga Pepeta, itawatambulisha wanamuziki wake wapya kwenye onyesho lao litakalofanyika Siku ya Wapendanao kwenye ukumbi wa Da’ West Park, Tabata.
Onyesho hilo ambalo limeandaliwa na Bob Entertainment na kudhaniniwa na Dodoma Wine na Freditto Entertainment litajulikana kama Dodoma Wine Valentine Show.
Mkurugenzi wa bendi hiyo, Asha Baraka, alisema jana kuwa siku hiyo ya Februari 14 ambayo huadhimishwa na wapendanao duniani kote, watatumia kutambulisha wanamuziki wapya waliojiunga na bendi hiyo hivi karibuni wakiwemo wanenguaji.
Hata hivyo, Asha hakuwataja wanamuziki wala wanenguaji hao, lakini amesema kuwa wanatoka kwenye bendi mbalimbali maarufu nchini.
African Stars Entertainmernt (ASET) ni taasisi ya muziki ambayo kazi yake ni kuandaa na kukuza wanamuziki. Ninawaomba wapenzi wajitokeze kwa wingi siku hiyo ili waone silaha zetu mpya pamoja na rap zetu mpya,” alisema Asha.
Asha alisema pia wanamuziki wake wamejiandaa vya kutosha kuburudisha mashabiki wao siku hiyo.

Tuesday, February 8, 2011

SAKATA LA VYUO NI KAZI KWELI KWELI!

BAADA YA WAZIRI MKUU WA FEDHA KUZUNGUMZIA POSHO WALIYOONGEZEA KWA WANAVYUO KWA KUPITIA MKONO WA SERIKALI. CHUO CHA MKWAWA LEO WAMEGOMA BAADA YA KAULI HIYO.
Hapa wanachuo wa mkwawa wakikusanyika kufanya mgomo huo

Saturday, February 5, 2011

vituko vya mwanangu fede.

Mtoto wa mkulima Ndani ya mkoa wa Iringa jana!

Dj Muba aleta utata....!!!!

Huyu ni moja kati ya maDj wakali na wanaoogopeka katika mji wa Iringa na Tanzania kwa ujumla ni kutokana na aumahiri alionao katika kuchezea mashine na kuwapagawisha mashabiki wa mziki.
 Hapa Dj Muba akiwa katika pozi.
Utata umetokana na jamaa kuonekana kushiriki kucheza na kujumuika kwa pamoja na mashabiki wa muziki hali ambayo haijazoeleka kwa baadhi ya madj waliona jina mjini! kitu ambacho kimewafanya mashabiki wake kuulizana kwamba ndiye au siye wanaomfahamu?

NAKIRI MAKOSA R MIX (www.bongo120.blogspot.com)

Friday, February 4, 2011

Tamasha la Mwalimu Nyerere Feb. 14

TAMASHA la filamu la Mwalimu Nyerere linatarajiwa kuanza kurindima kuanzia Februari 14 hadi 19 kwenye viwanja vya Leaders Club, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam juzi, Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF),
Simon Mwakifwamba, alisema ni mara ya kwanza kufanyika kwa tamasha hilo, ambalo litahusisha wageni kutoka Nollywood Nigeria, Afrika Kusini na Hollywood Marekani.
Alisema, siku hiyo ya ufunguzi, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete atazindua rasmi TAFF sambamba na tamasha hilo, ambalo zaidi ya filamu 20 zilizofanya vizuri za ndani na nje zitaonyeshwa.
Aidha, Mwakifwamba alisema, mbali ya kuwepo kwa filamu hizo pia kutakuwa na burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali likiwamo kundi la The African Stars ‘Twanga Pepeta’, FM Academia, Ambwene Yesaya ‘Ay’, Diamond, Khalid Mohamed ‘TID’, Mzee Yusuph, Lawrence Malima ‘Marlaw’, Albert Mangwea, Farid Kubanda ‘Fid Q’, Joh Makini na wengineo.
Aliongeza kuwa, katika siku za tamasha hilo kabla ya maonyesho ya siku husika, kutatunguliwa na mafunzo ya mada mbalimbali zinazohusiana na shughuli za filamu na maigizo kutoka kwa wakufunzi waliobobea.
Alisema, siku ya kufungwa kwa tamasha hilo, mgeni rasmi atatoa zawadi na tuzo kwa waasisi wa taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere na Rashid Kawawa ‘Simba wa Vita’ kwa mchango wao katika maendeleo ya taifa na tasnia ya filamu nchini.

Slow Down Zone.

Dj pirlo kwenye mixer!

Haya wajameni huyu nimoja kati ya wa2 ambao mimi ninawakubali! but sio mimi pekee ila mpaka uongozi mzima wa Pro24 Djs wamekiri hili kwamba jamaa anaye kwenda kwa jina la Dj Pirlo ni mkali wa kuchezea mashine zilizokwenda kidato na kuwafanya mashabiki wa muziki kupagawa! mbaya zaidi kijana huyu kutokana na umahiri wake uongozi huo wa Pro24 umeamua kumkabidhi kijana huyu mji wa Iringa ili wakazi wote wa Iringa watambue uwezo huo ninaouzungumzia na Nje ya hilo kijana huyu anayejulikana kwa jina la Dj Pirlo anajishughulisha na Moja ya Radio kali mjini hapa inayofahamika kwa Nuru fm 93.5 Mhz ni noumah!!!! kwa upatikanaji wake kwa maeneo ya Starehe mtafute ndani ya Club V.i.p utambue ukweli kuhusu hili! or check nae kupitia  manp88@hotmail.com chao!

Usafiri wa JK

Jamani! huu ndio usafiri anaotumia Raisi wetu anapoelekea kazini.

Thursday, February 3, 2011

Wenger amtetea Cecs kwa kauli ya Moyes

Meneja wa Arsenal Arsene Wenger, amemtetea Cesc Fabregas baada ya meneja wa Everton David Moyes kutoa madai kwamba nahodha huyo wa Gunners alipaswa kutolewa nje wakati wa mapumziko.
Arsene Wenger
Arsene Wenger
Everton walikuwa wakiongoza kwa bao 1-0 hadi kipindi cha kwanza, baada ya bao la utata lililofungwa na Louis Saha, aliyeonekana ameotea.
Lakini baada ya kupoteza mchezo kwa kufungwa mabao 2-1 katika uwanja wa Emirates, Moyes alisema: "Matamshi aliyoyatoa Fabregas kwa mwamuzi wa akiba na mwamuzi mwenyewe wakati wa mapumziko, alipaswa kutolewa nje kwa kadi nyekundu."
Hata hivyo Wenger alimtetea na kusema: "Fabregas hakuzungumza na mwamuzi wakati wa mapumziko, bali mimi ndiye nilizungumza naye."
Hasira zilipanda baada ya Saha kufunga bao la kwanza katika dakika ya 24 akiwa eneo ambapo mameneja wote walikiri alikuwa ameotea.
Hata hivyo, kwa mwamuzi Lee Mason kulikuwa na hamaki zaidi kwenye njia ya kuelekea vyumba vya kubadilishia nguo.
Moyes hakutaka kuzungumzia kile alichodai alisikia Fabregas akimwambia mwamuzi, lakini meneja huyo anahisi tukio hilo lilibeba matokeo ya mchezo.
"Nadhani kwa kutomtoa nje Fabregas kulibadili mtiririko wa mchezo," aliongeza Moyes.
"Nisingependa kutamka aliyoyasema Fabregas.
"Hayakuwa maneno mazuri kwa mtu mwenye hadhi na kipaji cha kusakata soka kama yeye.
"Kama angeyatamka maneno hayo uwanjani, angetolewa nje kwa kadi nyekundu."
Hata hivyo Wenger akimtetea nahodha wake alisema: "Nilikuwa karibu na Fabregas wakati wa mapumziko na sioni kwa nini David Moyes anamkasirikia."
Wenger alifurahishwa na moyo uliooneshwa na timu yake kuweza kurejesha bao na kupata la ushindi na kusema hali hiyo inaweza kuwasaidia katika mbio zao za kuutafuta ubingwa.
"Tupo tayari kwa mapambano ya kuwania ubingwa na tumeonesha hivyo kwa mara nyingine," Aliongeza Wenger.

Misri kazi balaa limerudi upyaaaaaaaaa..!!!!!

Wafuasi wa Rais wa Misri, Hosni Mubarak wamekabiliana na waandamanaji wanaomtaka kiongozi huyo aondoke madarakani katikati mwa mji wa Cairo.
Wafuasi na wapinzani wa Mubarak wakipambana
Wafuasi na wapinzani wa Mubarak wakipambana
Maelfu ya wafuasi wa Bw Mubarak walimiminika kwenye eneo la Tahrir na kuondoa vizuizi vilivyokuwa vimewekwa na waandamanaji.
Pande hizo mbili zilirushiana maneno kabla ya kuanza kurushiana mawe.
Jeshi ambalo awali lilitoa wito kwa waandamanaji kutawanyika na kurejea katika shughuli zao za kawaida bado halijaingilia kati.
Taarifa ambazo hazijathibitishwa zinasema maafisa wa polisi waliokuwa wamevalia kiraia walikuwa miongoni mwa baadhi ya wafuasi wa Bw Mubarak waliojitokeza katika eneo la Tahrir.
Mapambano mengine yameripotiwa kwenye mji wa Alexandria.

Joh Makini - Brand (www.bongo120.blogspot.com)

Wednesday, February 2, 2011

Tuesday, February 1, 2011

Mchakato uliendelea na ilikuwa kama hivi.

a
 Crement Sanga alishiriki kushauri ili mambo yaende sawa.
hoya unazingua ww!!!
hoya tafuta pozi lingine bana mpaka umshike huyo dada?
Hapa mambo yalianza kuwa magumu mpaka watu wakashika kiuno
nafikiri hukujua kama nilikuwa kazini that y! ukanicall! (kulia) D-zonger